“Mazeruzeru wanawindwa barani Afrika!” Vichwa vya habari kama hivi vimekuwa vya kawaida siku hizi. Vichwa hivi vya habari vinaleta mihemko mikubwa lakini kwa kweli vinaangazia uhalisia hakiki: kwamba katika baadhi ya nchi, mazeruzeru wanashambuliwa - kwa kawaida na mapanga na visu - kwa lengo la kupata viungo vya miili yao. Mashambulizi haya yana misingi yanayotokana na imani ya ushirikina ambamo inaaminika ya kwamba viungo fulani vya miili ya mazeruzeru vinaweza kuleta utajiri na bahati nzuri vinapotumiwa katika madawa ya wachawi. Jambo hili basi limesababisha uuzaji na ununuzi wa viungo vya mwili katika soko nyeusi, na hata, wakati mwingine, kumekuwa visa vya wizi katika makaburi ya maalbino au mazeruzeru. Viungo vya mwili vimeeripotiwa kuuzwa kwa mamia au maelfu ya dola za Marekani. Hakika, kama ni umaskini unaowafanya watu kuwashambulia wenzao ambao wako tofauti kwa sababu ya ulemavu wao wa ngozi, basi bei hizi za juu za sehemu hizi za mwili inaashiria kuwepo na ushirika wa watu wenye uwezo wa kifedha katika jamii.
Uzeruzeru ni hali ya maumbile ambayo husababishwa na upungufu mkubwa au kutokuwepo kwa melanin katika ngozi, nywele na macho. Kuna aina mbalimbali za ulemavu wa ngozi lakini ule unayojulikana zaidi - na ambao umesababishwa wale wenye uzeruzeru kuvamiwa - ni wakati ngozi yote, nywele zote na macho yote yameathirika kiwango cha kumfanya mtu aonekane tofauti katika familia na jamii yake. Ni lazima mama na baba wabebe jeni ya uzeruzeru ilikuweza kupitisha jeni hii kwa mtoto. Inaweza kurithiwa hata wakati wazazi wote wawili hawana hali hiyo. Katika hali hiyo, kuna asilimia 25 katika kila mimba ya kwamba mtoto atakuwa na uzeruzeru. Uzeruzeru kwa ujumla husababisha uharibifu wa maono kwa viwango tofauti katika kila mtu binafsi. Pia husababisha uathirikaji wa nguvu wa kupata kansa ya ngozi ambapo tahadhari ni duni au haipatikani kabisa. Idadi ya marudio ya uzeruzeru inatofautiana kwa kanda huku Amerika ya Kaskazini na Ulaya kuwa na takribani ya1 kati ya 17,000 walioathirika. Katika maeneo kadhaa ya Afrika kusini mwa Sahara, idadi ya marudio inaweza kuwa ya juu kama 1 kati ya 1,500. Hapa ndipo pia eneo ambamo mashambulizi yote ya kimwili yameripotiwa hadi sasa na mashirika ya kiraia yakiripoti mashambulizi juu ya 400 katika nchi 25 katika eneo hili. Hesabu hii ya mashirika haya yalianza mwaka wa 2007. Hizi tu ni kesi zilizoripotiwa; kuna uwezekano wa idadi halisi ya mashambulizi kuwa juu ya ile iliyoripotiwa.
Katika kukabiliana na mashambulizi hayo, Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa lilipitisha maazimio kadhaa kuanzia mwaka wa 2013 hadi sasa, wakilaani mashambulizi na kuonyesha ubaguzi ambao umesababisha mashambulizi hayo. Zaidi ya hayo, mwaka wa 2013, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu 'lilipitisha azimio muhimu mwaka wa 2013 (Azimio 263) wakiorodhesha hatua ambazo mataifa yanayohusika yanapaswa kuchukua ili kulinda mazeruzeru. Hivi karibuni, mwezi wa Machi mwaka wa 2015, Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) liliamrisha kuwepo na mamlaka ya mtaalamu huru anayeendesha kampeni,uhamasishaji,uelimishaji na uwezeshaji kuhusu haki za mazeruzeru; nilishika wadhifa huu mwezi wa Agosti 2015.
Flickr/MONUSCO Photos (Some rights reserved)
An albino girl and her mother are photographed in Kinshasa, RD Congo. Despite the frequency of Albinism in Sub-Saharan Africa, civil society reports over 400 documented attacks across 25 countries in the region since 2007.
Kuna uwezekano wa kubadilika kwa ndoto yangu na aula zangu kuhusu mamlaka hii ninaposhauriana na watu wengi na pia ninapopata habari mpya. Huku ninapotumaini kushughulikia vikwazo dhidi ya haki za binadamu za watu wenye uzeruzeru duniani kote, aula yangu kwa miaka 3 ijayo itakuwa katika kanda ya Afrika kusini mwa Sahara na msisitizo wa kukomesha mashambulizi na maswala yanayotokea.
Nitafanya kazi na mataifa yaliyoathirika kuweka hatua maalum ambazo zinaweza kumaliza mashambulizi haya na masuala yanayohusiana.
Aula ya kwanza ni lazima mashambulizi yasitishwe. Hili ni jambo la dharura. Nitafanya kazi na mataifa yaliyoathirika kuweka hatua maalum ambazo zinaweza kumaliza mashambulizi haya na masuala yanayohusiana kama vile biashara inayohusu viungo vya mwili na ufungamanishaji upya katika majumuia mitaani mwa wale waliokimbizwa kutoka kwa makazi yao kwa sababu ya mashambulizi hayo. Mkutano wangu wa kwanza mwaka huu wa 2016 utakuwa wa kuendeleza hatua hizi maalum.
Pili, kuna haja ya kushughulikia mahitaji ya huduma za afya yanayowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi. Kansa ya ngozi huua idadi kubwa ya watu hawa kabla ya wao kufika umri wa miaka 40 katika baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini mwa Sahara. Hii inatokana na ukosefu wa taarifa kuhusu huduma na ulinzi wa ngozi, na pia ukosefu wa upatikanaji wa mafuta ya kulinda ngozi dhidi ya mionzi ya jua na mavazi ya kukinga ngozi dhidi ya mionzi ya jua. Pia ni kwa sababu wale wenye ulemavu wa ngozi hulazimika kufanya kazi nje baada ya kushindwa kupata elimu ambayo ingewawezesha kupata ajira ambayo hufanyika ndani ya nyumba. Kiasi cha wale wanaoacha kuenda shuleni ambao ni mazeruzeru katika baadhi ya nchi inahusiana na uharibifu wa maono yao na ukosefu wa kuchukuliwa kwa hatua zozote zinazoridhisha za kuwalinda. Kiasi cha wale wanaojiondoa shuleni pia kimechochewa zaidi na unyanyapaa na ubaguzi. Nitafanya kazi na mataifa na wadau muhimu kutoka mashirika ya kiraia na kuwa na vikao vya afya katika bara zima ili kubaini hatua endelevu ambazo zinaweza kutekelezwa ili kuwezesha masuala hayo kushughulikiwa.
Tatu, natumai nitabainisha njia bora za kusaidia na kulinda mazeruzeru, na kukusanya njia hizi bora kuwa sera mfano wa kuigwa. Sera huangazia hatua za haraka ambazo mataifa yanaweza kutimiza na z inaweza kuwa na ufanisi katika kuleta mabadiliko ya haraka. Sera hii itakuwa waraka hai ambayo ninatumai kuiboresha ninapozidi kupata taarifa mpya zinazokuja kutoka kwa ripoti mbalimbali na pia kutokana na utafiti ninayofanya. Inatarajiwa ya kuwa mataifa hatimaye yatatohoa sera hii ili iwe kama kijalizo kwa sheria zingine ambazo zinashughulikia watu wenye uzeruzeru kama vile sheria zinazosimamia watu wenye ulemavu, na sheria zinazoshughulika na upataji wa huduma bora zaidi ya afya. Sera itashughulikia masuala yote yanoyoibuka kila siku yanayohusu uzeruzeru, zaidi ya suala la mashambulizi na kwa hiyo itahusisha masuala ya sekta mbalimbali za vyombo vya serikali na zisizo za kiserikali.
Utafiti nitakaofanya kama Mtaalamu Huru utakuwa unaendelea ili kuboresha ubora na wingi wa taarifa zilizopo kuhusu haki za binadamu za watu wenye ulemavu wa ngozi. Itahusisha pia kazi ya kubaini mfumo wa kisheria ambao unaweza kutoa mfumo endelevu na madhubuti ya kulinda mazeruzeru. Utafiti huo utajaribu kutafuta sababu kuu za mashambulizi, kuanza na suala la uchawi. Hatimaye, kazi yangu itakuwa ni pamoja na utetezi, na uhamasishaji wa suala hilo, hasa kwa njia ya matumizi ya vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vya kijamii.
Ninaona uanzishaji wa mamlaka ya Mtaalamu Huru wa ulemavu wa ngozi kama usemi mkubwa wa mapenzi ya pamoja ya Baraza la Haki za Binadamu: kumaliza mashambulizi dhidi ya mazeruzeru na kufanya kazi katika kutafuta sababu kuu ya mashambulizi haya. Lengo ni lazima liwe la kuanzisha hatua za kuzuia mashambulizi dhidi ya watu hawa. Ilikutimiza malengo haya yote kwa kutumia mamlaka niliyopewa, nitahusisha wadau mbalimbali katika mikoa yote hususan katika maeneo ya walioathirika na mashambulizi dhidi ya mazeruzeru. Aidha, ningependa kusisitiza haja yangu ya kuungana na kusaidiana na mataifa yaliyoathirika mahsusi kwa kujiingiza katika kuelewa sababu kuu na kutekeleza hatua ya kuzuia mashambulizi haya. Mwishowe, ningependa kusisitiza jukumu la asasi ya mashirika ya kiraia, hasa mashirika yasiyo ya kiserikali na wasomi kwa kunipa habari na kwa kuwa chanzo cha ushiriki wenye ufansisi katika kuniwezesha kuendesha kampeni,uhamasishaji,uelimishaji na uwezeshaji kuhusu haki za mazeruzeru.